Jeshi la Polisi mkoani Singida, limefanikiwa kukatama watu watatu wakazi wa kijiji cha Makoleo kata ya Kilangali tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni, kwa tuhuma ya kumiliki kinyume na sheria bunduki tatu aina ya gobore zikizokuwa wanazitumika kwenye matukio ya uhalifu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Debora Daud Magiligimba, watuhumiwa hao wamekamatwa Machi mosi mwaka huu, saa tano asubuhi katika kijiji cha Makoleo.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Lugadila Ruponya (42),Solomoni Dotto (25) na Emmanuel Paul (25).
Akifafanua, alisema magobore mawili yamekamatwa kwa mtuhumiwa Lugadila akiwa amweyaficha chumbani kwake katika nyumba anayoishi. Gobore jingine limekamatwa kwa mtuhumiwa Solomon, akiwa ameficha nyumbani kwake.
“Upatikanaji wa silaha hizo pamoja na ukamatwaji wa watuhumiwa hao,unatokana na msako mkali uliofanywa na jeashi la polisi likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mnazimoja. Msako huo ulifanyika baada ya kutokea kwa tukio la uporaji katika kijiji hicho machi mosi mwaka huu saa nane usiku,” alisema kamanda huyo.
“Watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumba ya Logo Jilala (38). Baada ya kuingia ndani walimkatakata kwa panga mgongoni Logo na kufanikiwa kumpora shilingi 1,290,000 taslimu na simu ya kiganjani yenye thamani ya shilingi 40,000,” alisema.
Kamanda Magiligimba,alisema wanaendelea na uchunguzi wa kina, ili kuweza kuwakamata watuhumiwa wengine watatu waliofanikiwa kutoroka. Pia kutafuta mtandao huo wa uhalifu.
Katika hatua nyingine, alisema wafanyabiashara wawili wa mjini hapa ambao wamekataa kutajwa kwenye vyombo vya habari, wamesalimisha polisi pombe za viroba mbalimbali vyenye uzito wa robo tani vilivyopigwa marufuku.
“Nitoe wito kwa wafanyabiashara wenye pombe za viroba vilivyopigwa marufuku, kuvisalimisha mapema kwenye vituo vya jeshi la polisi,kama njia moja wapo ya kutii sheria bila shurti,” alisema Magiligimba.
Sign up here with your email