MWANA WA TSHISEKEDI KUONGOZA UPINZANI DRC - Rhevan Media

MWANA WA TSHISEKEDI KUONGOZA UPINZANI DRC

Felix Tshisekedi kuongoza upinzani DRCHaki miliki ya pichaAFP
Image captionFelix Tshisekedi kuongoza upinzani DRC
Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo umemteua mwana wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa muungano huo Etienne Tshisekedi, ili kumrithi babake.
Felix Tshisekedi atakuwa rais wa muungano wa vyama tisa vinavyompinga rais Joseph Kabila.
Uteuzi wake ulitangazwa licha ya pingamizi kutoka kwa makundi mawili kwenye muungano huo.
Kiongozi wa muda mrefu wa muungano huo Etienne Tshisekedi, alikuwa ameuongoza kwenye mazungumzo ya mwezi Disemba kuhusu wadhifa wa urais.
Kwenye makubaliano yaliyoafikiwa, bwana Kabila ataondoka madarakani baada ya uchaguzi ambao utafanyika mwaka huu.
Muhula wake wa pili madarakani ulikamilika rasmi Disemba iliyopita.
Kifo cha bwana Tshisekedi kilizua ghasia za mwezi mmoja kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama mjini Kinshasa, na kusababisha taharuki ndani ya upinzani.
Etienne Tshisekedi alifariki mwezi mmoja uliopitaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEtienne Tshisekedi alifariki mwezi mmoja uliopita
Previous
Next Post »