Wananchi 246 wa Zimbabwe wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana na mvua ambazo zilikuwa zikinyesha nchini humo tangu mwezi Desemba hadi sasa na kusababisha mafuriko.
Hilo limethibitisha na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Saviour Kasukuwere ambapo alisema licha ya watu hao kupoteza maisha wananchi wengine 128 walijeruhiwa kutokana na mafuriko hayo.
Kasukuwere alisema katika mafuriko hayo pia yamesababisha karibu watu 2,000 kupoteza maisha na hivyo msaada wa haraka unahitajika ili kuwasaidia wananchi wote waliopata athari.
“Kuna upungufu wa mahema, vyakula na madawa kwa ajili ya watu ambao wameathirika na mafuriko,”Kasukuwere aliliambia gazeti la The Herald na kuongeza, “Kunahitajika mablanketi na nguo nguo kwa familia zilizoathirika na wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa homa ya mapafu (pneumonia).”
Sign up here with your email