Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira )January Makamba
Arusha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira )January Makamba amesema Monduli ni moja ya wilaya zitakazonufaika na mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ili kuwasaidia wafugaji wanaohamahama na kusababisha uharibifu wa mazingira.
Monduli ni moja ya wilaya zinazokumbwa na ukame hali inayosababisha wakazi wa eneo hilo ambao kwa asilimia kubwa ni jamii ya wafugaji kuhama kutoka sehemu hadi nyingine kutafuta malisho.
Amesema mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa wafugaji kupata malisho bora kwa ajili ya mifugo yao ili kupunguza changamoto ya kuhama hama.
Makamba amesema hayo leo wakati akipokea taarifa ya hali ya mazingira katika wilaya ya Monduli alipokwenda kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira katika ziara yake ya mikoa mbalimbali
Sign up here with your email