Dar es Salaam. Chama cha wafanyakazi wa majumbani na hotelini Tanzania(Chodawu) kimeiomba serikali na wananchi kuungana kwa pamoja ili kuweza kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na kuwatambua kama wafanyakazi wengine.
Hayo yamesemwa leo (jumanne) na mratibu wa Chodawu kanda ya Afrika Vicky Kanyoka wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kanyoka alisema wafanyakazi wa ndani bado wameendelea kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo viovu kinyume cha Sheria.
"Wafanyakazi wa ndani wanapewa mshahara usiokidhi mahitaji yao,wanapigwa,wanasafirishwa nchi za uarabuni na kufanyishwa kazi kinyume na matarajio yao,wakiitwa majina ya ajabu,wanapigwa na kubakwa." alisema Kanyoka
Sign up here with your email