Maafisa wa serikali nchini Nigeria wanasema magunia matano yaliyokuwa na mabunda ya noti yamegunduliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kaduna.
Pesa hizo zilipatikana katika dawati la kuhudumia wasafiri wanaoingia uwanja wa ndege kuabiri ndege.
Fedha hizo, za thamani ya jumla ya dola 150,000 za Marekani, ziligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida wa mizigo uwanja wa ndege.
Msemaji wa tume ya uhalifu wa kifedha nchini Nigeria Wilson Uwujaren amesema magunia hayo yalikuwa na mabunda ya noti mpya za naira 200 na 50, ambayo yalikuwa bado hayajafunguliwa kutoka kiwandani.
Amesema uchunguzi unaendelea kubaini nani mwenye magunia hayo.
Mabunda hayo ya noti yalikuwa yamefungwa na kuwekwa utepe kuonesha yalikuwa yametoka kwa kampuni ya kufua sarafu ya Nigeria Security and Minting Plc (NSPM).
Ibrahim Bappah anayefanya kazi katika afisi ya kupambana na rushwa Kaduna alisema noti hizo mpya ziligunduliwa wakati wa ukaguzi baada ya "harufu nzuri ya kipekee" kutambuliwa.
Magunia hayo yenye pesa yalikuwa yameachwa bila mtu wa kuyatunza na hayakuwa na nembo za kumtambua mwenyewe.The bags were left unattended and without tags.
The EFCC is investigating whether it was an illegal attempt to move money.
Sign up here with your email