Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii wa 'hip hop', Joseph Haule (Profesa Jay) amesema hana kinyongo na wasanii wote waliokwenda jimboni kwake kipindi cha uchaguzi oktoba 25, 2015 kwa ajili ya kumpinga.
Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii instagram ameandika maneno machache yanawagusa moja kwa moja wasanii wenzake waliokuwa nje ya chama hicho kuwa amewasamehe ila amewataka wajiongeze kwa maana sanaa inahitaji umoja.
"Nilishawasemehe wasanii wenzangu waliokuja jimboni kupinga Ubunge wangu mabasi kwa mabasi, jiongezeni wanangu. Asante wana Mikumi kwa kuwa na imani kwangu, sanaa yataka umoja nitakubeba ukianguka". Ameandika Profesa Jay
Kwa upande mwingine msanii huyo amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wake wakae tayari kupokea mzigo mpya siku ya kesho Jumatano unaotarajiwa kupewa jina la 'kibabe'.
Sign up here with your email