Majambazi wenye silaha waliojifanya kuwa polisi wamevamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuiba, ripoti zimesema.
Inasemekana majambazi hao waliendesha gari lao mpaka eneo linalozuiwa kuingia na kuchukua makasha ya pesa taslimu.
Makadirio ya pesa zilizoibiwa yanatofautiana, lakini taarifa zinasema kuwa mamilioni ya dola ya sarafu za tofauti tofauti yameibiwa .
Kampuni zinazohudumu katika uwanja wa ndege wa OR Tambo, wenye shughuli nyingi barani, zimethibitisha kwamba wizi huo umefanyika.
"Hakuna miliyo ya risasi wala majeruhi walioripotiwa kutokana na tukio hilo. Majambazi walitoroka ‚" Kampuni ya viwanja vya ndege ya Afrika Kusini imesema katika taarifa yake, kulingana na taarifa za mtandao wa habari wa TimesLive.
Kikosi maalum cha polisi - Hawks, kimekataa kutoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo.
- Vurugu zatawala bungeni, Afrika kusini
- Wanafunzi warushiwa maguruneti SA
- Mahakama yaizuia Afrika Kusini kujiondoa ICC
Lakini chanzo kimoja cha habari ndani ya kikosi hicho kimeuelezea wizi huo ''kama kitu kilichoandikwa na kutekelezwa kama filamu ya Hollywood ", alikieleza kipindi cha BBC cha Newsday mwandishi wa Afrika Kusini Graeme Hosken.
Mwandishi huyo wa habari aliongeza kuwa wezi hao ambao walitumia njia maalum ya kuingia ndani ya uwanja wa ndege , walifahamu fika ni aina gani ya kasha la kuchukua na walikuwa makini kutochukua noti ndogo ambazo zingekuwa rahisi kuchukua.
Msemaji wa polisi, Athlenda Mathe, amenukuliwa na mtangazaji wa kitu cha Afrika Kusini eNCA akisema kuwa hawezi kutoa kauli '' juu ya kiasi cha pesa kamili zilizoibiwa".
Walinzi kutoka kampuni ya kibinafsi wanaolinda mali za thamani walizuiliwa na majambazi hao waliokuwa wakisafiri katika gari lenye nembo ya "polisi", TimesLive lilisema.
Kumekuwa na taarifa kuhusu wizi wa mizigo mingine ya thamani katika miaka ya hivi karibuni kwenye uwanja huo wa ndege.
Sign up here with your email