Afrika kusini imetupilia mbali mpango wake wa kuondoka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.
Hii ni baada ya mahakama kuu kuamua mwezi uliopita kuwa hatua ya serikali ya kujiondoa ilikuwa kinyume na katiba.
Afrika kusini ilikuwa imeshauri Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wake wa kuondoka ICC ikisema kuwa mahakama hiyo ilikuwa ikiaka 'mabadiliko ya uongozi'.
Hatua hiyo ilijiri baada ya ziara ya rais wa Sudan Omar al-Bashir nchini Afrika Kusini mwaka 2015.
Utawala chini humo ulikataa kumkamata bwana Bashir, licha ya yeye kukabiliwa na waranti wa ICC wa kutaka akamatwe kufuatia madai ya uhalifu wa kivita.
Bwana Bashir alikuwa akihudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika mjini Johannesburg, wakati serikali ilipuuza ombi la ICC la kumkata.
Gambia chini ya rais mpya Adama Barrow, hivi majuzi nayo ilifuta hatua yake ya kujiondoa ICC.
Sign up here with your email