KIMENUKA TRA YATIA KUFULI OFISI ZA TFF WAFANYAKAZI WATOLEWA NJE - Rhevan Media

KIMENUKA TRA YATIA KUFULI OFISI ZA TFF WAFANYAKAZI WATOLEWA NJE

Tokeo la picha la ofisi za tff


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na deni kubwa la kodi na la muda mrefu.
Zoezi hilo limefanyika mchana wa leo chini ya Kampuni ya Udalali na Minada ya Yono, ambayo kwa sasa ndiyo inazishikilia ofisi hizo baada ua kuwatoa nje wafanyakazi wote wa TFF na kuwataka waache kila kitu ndani.
Hakuna Ofisa wa TRA aliyekuwa tayari kuzungumza haraka wakati wa zoezi hilo leo mchana, lakini habari zinasema ni madeni ya tangu uongozi uliopita, chini ya Rais Leodegar Tenga kabla ya uongozi wa sasa, chini ya Rais Jamal Malinzi.
Na deni kubwa zaidi linatokana na kodi za mishahara ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazil Maximo kwa miaka minne tangu 2016 hadi 2010.
Deni lingine linalosababisha ofisi za TFF kufungwa ni la kodi ya Ongezeko la Thamani (VaT) la ziara ya timu ya taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njiani kwenye Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alipotafutwa Rais wa TFF, Jamal⁠ Malinzi alisema; “Ni kweli nasikia hilo limetokea na ni kwa sababu ya madeni ya kodi za mishahara ya ⁠⁠⁠Maximo na VaT ya mechi ya Brazil,”.
Malinzi akaongeza kwamba kutokana na tatizo hilo, msafara wa Tanzania uliokuwa unaelekea kwenye mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka (CAF) ambao kwa sasa upo Addis Ababa ukisubiri kuunganisha ndege kesho urudi Tanzania.
“Msafara wa Tanzania uko Addis Ababa na kesho ni uchaguzi mkuu CAF na pia itapigwa kura ya Zanzibar kupewa uanachama wa CAF na Tenga kuingia FIFA, msafara inaabidi urudi na kuacha yote haya,”amesema Malinzi. 
Pamoja na haya, suala hili litaathiri mambo mengi ikiwemo maandalizi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa ajili ya fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.
Na si ajabu operesheni zote za soka ya Tanzania zikasimama kwa muda iwapo TRA itaendelea kuzifungia ofisi za TFF.
Previous
Next Post »