KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA SERIKALI KUWA MFANO KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL - Rhevan Media

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA SERIKALI KUWA MFANO KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL

 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Prof. Norman Sigala na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kushoto). Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kulia) alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Taasisi za Serikali na Mashirika yote ya Umma kutumia kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Data Centre)chenye hadhi ya juu kabisa katika viwango vya ubora na usalama wa Taarifa na Kumbukumbu. 

Kamati pia imezitaka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia Kituo hicho katika kutunza kumbukumbu zake ili kuwa mfano kwa Taasisi nyingine za Umma. 

Akizungumza katiko maazimio ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mara baada ya ziara ya siku moja ya Kamati hiyo kuitembelea Kampuni ya Simu Tanzania TTCL pamoja na miradi ya Mkongo wa Taifa na Kituo Mahiri cha kutunzia kumbukumbu (Data Centre), Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Norman Sigala amesema, uhai wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL upo mikononi mwa Serikali ambayo ina jukumu kubwa la kuihusiha Kampuni hiyo yenye uwekezaji mkubwa. 

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imezitaka Taasisi zote za Umma na binafsi kulipa madeni zinazodaiwa na TTCL kuiwezesha Kampuni hiyo kujiendesha kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na Watendaji wa Umma wanaogharamiwa huduma za Mawasiliano kutumia huduma za simu za TTCL katika maeneo yote yenye huduma hizo. 

Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe Rita Kabati amesema, kukamilika kwa Mchakato wa kuondoka kwa Bharti Airtel ndani ya TTCL kunahitaji kwenda sambamba na uwezeshaji wa mtaji kama ilivyofanyika kwa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambazo sasa zinafanya vizuri.


Previous
Next Post »