Hatimaye zile kelele za mashabiki wa Yanga kuhusu suala la kuwasajali wachezaji muhimu wa Simba ambao mikataba yao ilikuwa inaelekea ukingoni ambao wameamua kukata mzizi wa fitini kwa kuongeza mikataba mipya katika klabu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara
Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema kuwa wachezaji hao Ibrahim Ajibu na Jonas Mkunde wamekubali kusaini miktaba ya miaka miwili kila moja huku ikiwa na vipengele ambavyo vinawaruhusu endapo watapata timu nje ya nchi wataruhusiwa kwenda kusaka maisha mapya.
Kuongeza mikataba ya wachezaji hao kumezima tetezi za kujiunga na watani zao Yanga ambao wapo katika kipindi kigumu kwa sasa kutokana na Mwenyekiti wao Yusuf Manji kuwa chini ya Ulinzi kwa tuhuma za kutumia Madawa ya kulevya na kusababisha account zake kufungiwa na Serikali.
Pia ni habari nzuri kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo ambao wana kiu ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu bara ambao wameukosa kwa miaka mingi.
Sign up here with your email