VIDEO:SIMBA YA POKELEWA KAMA MFALME WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA, IKIELEKEA KUIVAA MAJIMAJI - Rhevan Media

VIDEO:SIMBA YA POKELEWA KAMA MFALME WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA, IKIELEKEA KUIVAA MAJIMAJI

AAAAAA

Mashabiki wa Timu ya SIMBA SC wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu yao ikitokea Dar , Mashabiki wa Simba hawakujali kuwa ni usiku walichokiona wao ni kuipokea timu yao kwa furaha , shangwe huku wengine wakiimba aungurumapo simba hucheza nani …..? pamoja na kuiombea ushindi wa nguvu.

Simba inakuja kucheza na Maji Maji ( Wanalizombe) tarehe 04 katika uwanja wa MAJI MAJI uliopo mjini Songea mkoani Ruvuma.

Utakuwa mchezo mkali na wa hatari sana maana simba inahitaji ushindi iweze kurudi juu na kushika msukani huku Maji Maji wakipambana kuhakikisha wanapanda juu zaidi ili waweze kunusurika na kushuka daraja , PATAMU HAPO PICHA INAENDELEAAAA………

Umati wa mashabiki wa Simba katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Tumekusogezea na VIDEO ya mapokezi ya Simba usiku huo huo katika wilaya ya Tunduru .HABARI KWA HISANI YA www.ruvumatv.com



About Alex


Previous
Next Post »