MAANDAMANO DHIDI YA SERIKALI YAFANYIKA ROMANIA - Rhevan Media

MAANDAMANO DHIDI YA SERIKALI YAFANYIKA ROMANIA

Waandamana dhidi ya serikali RomaniaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWaandamana dhidi ya serikali Romania
Polisi nchini Romania, wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu wanaoandamana dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Bucharest.
Maandamano hayo yametajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa utawala wa kikomunist mwaka 1989.
Ripoti zinasema hadi watu elfu mia mbili na hamsini, wameandamana kupinga amri ya dharura iliyotolewa na serikali kuhalalisha baadhi ya makosa ya ulaji rushwa.
Mataifa sita yakiwemo, Ujerumani, Ufaransa na Marekani yametoa taarifa ya pamoja kuionya Romania dhidi ya amri hiyo yakisema huenda ikahujumu sifa yake kimataifa na mahusiano ndani ya EU na NATO.
Previous
Next Post »