Serikali imetangaza mwongozo mpya wa usanifu na ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache hususani vijijini ambao utasaidia kupunguza gharama za ujenzi .
Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, alisema mwongozo huo unatoa maelekezo kwa wanaotengeneza barabara za vijijini.
Nyamhanga alisema mwongozo huo utasaidia kupunguza gharama za ujenzi na usalama wa barabara tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanatumia gharama kubwa.
“Kipindi cha nyuma Wizara ilikuwa inatumia miongozo ya barabara kuu na za Mikoa na miongozo hii ina gharama kubwa kutokana na kukosa mwongozo wa barabara zinazopitisha magari 300 kwa siku hivyo kuepuka gharama hizi tukaanda muongozo huu,”alisema Mhandisi Nyamhanga.
Aidha aliwataka wahandisi na mafundi ujenzi watumie mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.
ALiongeza kuwa, barabara za vijijini zilikuwa hazina miongozo hivyo walikuwa wanatumia miongozo ya barabara hizo ambazo kwa siku zinapitisha magari 20,000 hadi 15,000.
Sign up here with your email