Mwanamke mmoja kutoka jimbo la Oregon alifanikiwa kumuingiza nyoka wake katika ndewe kabla ya nyoka huyo kukwama.
Ashley Glawe alichapisha picha yake katika mtandao wa facebook akiwa hospitali.
Aliandika: Kilikuwa kisa cha kushangaza sana katika maisha yangu baada ya nyoka wangu kuingia katika tundu ya sikio langu .
Alichapisha katika ujumbe huo katika mtandao akisema anamshikilia nyoka huyo kwa jina Bart baada ya kuingia katika ndewe yake ya sikio.
''Lilikuwa tukio la haraka hadi sikuweza kujitetea''.
Anasema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu nyoka wake lakini hakuna tatizo lolote kufikia sasa.
Aliwaambia marafiki zake mtandaoni kwamba madaktari walidunga sindano sikio lake na kulituliza, wakapanua ndewe hiyo kabla ya kumtoa nyoka huyo.
Nyoka huyo kwa sasa anadaiwa kuwa kati hali nzuri.
Sign up here with your email