Haki miliki ya pichaAFPImage captionRais Adama Barrow
Mbwa aliyemuuma na kumuua mtoto wa rais wa Gambia Adama Barrow ameuawa.
"Tuliamua kuwa haikuwa vyema kumruhusu mbwa huyu kuendelea kuzururu barabarani. Tulimfanyia uchunguzi na kubain ikuwa hakuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa," taarifa kutoka wizara ya kilimo zilisema.
Mtoto huyo wa umri wa miaka minane Habibu Barrow, aliripoptiwa kuaga dunia akiwa njiani kuenda hospitalini eneo la Manjai karibu na mji mkuu wa Gambia Banjul.