1.NI WAKATI GANI WANATAKIWA KULINDWA.
Ni ule wakati ambao marehemu ameacha mali lakini bado hajapatikana msimamizi wa mirathi kwa ajili ya kusimamia mali hizo huku kukiwa kuna watoto wanaohitaji mahitaji muhimu kutoka katika mali hizo. Pengine hajapatikana msimamizi wa mirathi kwakuwa kuna mgogoro mahakamani, au ndugu hawaelewani, au msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa hajulikani alipo, au kuna utata katika wosia n.k.
Chochote kile ambacho kitasababisha msimamizi wa mirathi achelewe kupatikana basi ujue ni wakati huo ambapo mahitaji na maslahi ya mtoto yanatakiwa kulindwa.
2. YAPI MAHITAJI YA WATOTO WADOGO.
Mahitaji ya watoto wadogo ni kama ada za shule, mavazi, matibabu, na kila ambacho ni muhimu kwa ustawi wa mtoto. Na kwa suala la ada mtoto si lazima awe mdogo sana bali hata wale wa kidato cha tano, sita, chuo nao waweza kuwa watoto ambao maslahi yao ni muhimu kulindwa .
3. WATOTO WANAOSTAHILI KULINDWA.
Watoto wanaostahili kulindwa ni wale ambao watakuwa ni warithi halali wa marehemu. Ni wale ambao hakuna mgogoro kuwa ni warithi au si warithi. Aidha ikiwa kuna mgogoro kama watoto au mtoto fulani ni mrithi halali au si mrithi basi pia unaweza kuomba kulinda maslahi yake ambapo mahakama itaamua ikiwa anastahili au hastahili.
4. NINI UFANYE KULINDA MAHITAJI YA WATOTO.
( a ) Mtu yeyote mwanafamilia, ndugu, mzazi aliyebaki,mlezi anatakiwa kupeleka maombi mahakamani akiiomba mahakama kusimamia baadhi ya mali kwa muda ili kupata mahitaji ya watoto wakati wakisubiri utatuzi wa mgogoro katika familia.
Sign up here with your email