Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Gwanseri wilayani Muleba kuuawa na baba yake wa kambo kisha kumfukia ndani ya nyumba akiwa amemuweka kwenye mfuko wa plasitiki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amesema tukio la mwanafunzi huyo kuuawa lilitokea jana katika kijiji cha Karutanga wilayani Buleba na kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remijius Poncian(16).
Kamanda Olomi amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni baba wa kambo, Hassan Misigaro (52) anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Sign up here with your email