ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMDHALILISHA MTOTO - Rhevan Media

ATUPWA JELA MAISHA KWA KUMDHALILISHA MTOTO

Tokeo la picha la MAHABUSU



Chunya.Mkazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi wilayani hapa, Robert Francis (19) amehukumia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (4) na kumsababishia maumivu makali.
Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2017 kwa mara ya kwanza ilifikishwa mahakamani hapo Januari 16 na upande wa Jamhuri ulileta mashahidi wanne ambao walitoa ushahidi wao na hatimaye hukumu kusomwa leo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Chunya, Osmund Ngatunga alisema ushahidi wa daktari na mtoto ndio unamtia hatiani mshtakiwa huyo.
Alisema mahakama inamtia hatiani na kumpeleka jela maisha kutokana na vitendo hivyo kudhalilisha sana watoto licha ya kuwapo sheria kali.








Previous
Next Post »