WAZIRI NAPE AMPONGEZA SIMBU, ASEMA SASA TANZANIA INARUDI - Rhevan Media

WAZIRI NAPE AMPONGEZA SIMBU, ASEMA SASA TANZANIA INARUDI

QCOWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, mhe, Nape Nnauye (Mb), amesema mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania, aliyeshinda medali ya dhahabu hivi karibuni huko nchini India, Alphonce Simbu, amefungua njia ya kufanya vizuri zaidi kwa wanariadha wengine na kuirudisha Tanzania katika ramani ya mchezo huo ulimwenguni kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita.

Waziri Nape aliyasema hayo wakati wa hafla maalumu ya kumkaribisha na kumpongeza mwanariadha huyo, iliyoandaliwa na kampuni ya Multchoice tanzania mabao pia wamekuwa wamkimdhamini mwanariadha huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Waziri Nnauye alisema kuwa ni fahari kubwa kwa Tanzania na furaha ya kila mmoja kuona kuwa sasa anapatikana mtu aneyonyesha matumaini ya kuirejesha Tanzania katika enzi za kuitikisa dunia katika michuano ya riadha hapa ulimwenguni kama ilivyokuwa hapo zamani
“Tunafurahi kuona kuwa, hatimaye baada ya miaka mingi ya kutofanya vizuri katika michuanao mbalimbali ya riadha sasa tuna mtu anaeweza kututoa kimasomaso na hii ni changamoto kwa wanariadha wengine kufanya vizuri katika michuano ijayo” Alisema Nnauye
“Yapo mashindano mengine yaliyo mbele yetu ambayo yatafanyika Uganda hivi karibuni, tunaahidi kulisaidia shirikisho la riadha Tanzania ili tuweze kufanya vizuri na hatimaye kuitangaza nchi yetu” Aliongeza
Alphonce Simbu anedhaminiwa na kampuni ya Multchoice Tanzania, alishinda medali ya dhahabu hivi karibuni kwenye mashindano yajulikanayo kama, Standard Chartered Mumbai Marathon, yaliyofanyika nchini India akiwaangua mamia ya wanariadha kutoka katika nchi marufu zinazoongoza katika mchezo huo ulimwenguni kama Kenya na Ethiopia.
Awali akimkaribisha waziri, kaimu mkurugenzi wa Multchoice Tanzania, Baraka Shelukindo, alisema wamekuwa wakimdhamini mwanariadha huyo kama sehemu ya mkakati wa kuinua riadha na kuonyesha uzalendo kwa kwa taifa
Previous
Next Post »