Kinara mkuu wa
vuguvugu la waasi nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama, ametangaza
usitishwaji wa mapigano kwa kipindi cha miezi miwili, huku akiongeza
siku saba za mazungumzo ya amani, yalioanza msimu wote wa siku kuu ya
krismasi.
Kinara huyo mkuu wa Vuguvugu la Renamo, na
aliyechaguliwa kuwa kiongozi rasmi wa upinzani, aliongoza vita dhidi ya
serikali ya Frelimo wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini
Msumbiji, ambayo yalimalizika mwaka 1992. Hata hivyo mwaka jana, taharuki iliibuka tena na kumeshuhudiwa mapigano na mauwaji ya viongozi wa kisiasa.
Bwana Dhlakama sasa anaishi mafichoni katika maeneo ya milima katikati mwa nchi hiyo.
Sign up here with your email