Makundi kadhaa ya
waasi nchini Syria yamesema kuwa yamesimamisha mashauriano ya kupanga
mkutano wa amani unaoandaliwa na Urusi na Uturuki kufanywa katika nchi
ya Kazakhstan mwezi huu, yakilaumu Serikali kwa kuvunja mapatano ya
kusitisha mapigano kwa siku nne.
Waasi hao wanasema walikuwa
wameheshimu mapatano hayo lakini wanajeshi wa serikali ya Syria na
washirika wao wa Irani wamekiuka mwafaka huo mara kadhaa.Waasi hao wanasema maeneo yaliyoshambuliwa bila kujali ni kama vile Ghouta na Wadi Barada, maeneo hayo yote yakiwa karibu na Damascus.
Waasi hao wanashikilia Wadi Baradi, ambalo ni eneo muhimu sana kwa maji yanayowashughulikia wakaazi wa Damascus.
Waasi wamelaumu Serikali kwa kuyachafua maji kwa kutumia dizeli.
Sign up here with your email