UZINDUZI WA VIFAA VIPYA VYA KUFANYIA KAZI BANDARINI ZANZIBAR - Rhevan Media

UZINDUZI WA VIFAA VIPYA VYA KUFANYIA KAZI BANDARINI ZANZIBAR



 Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena na Mizigo mizito leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo  Makontena ya mizigo mizito,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,(kushoto) Makamo wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bandari Bw.Salmin Senga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo  Makontena ya mizigo mizito wakiwepo na Viongozi mbali mbali,  ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mashine ya 
 ​Reach
  
 ​Stacker ​
 yenye uwezo wa kunyanyua Tani 
 ​45
  ikionesha namna inavyoweza kufanya 
 ​kutoa huduma 
 Makontena 
 ​baada ya kushushwa ​
 katika Meli 
 ​ 
 na kupanga sehemu ya kuhifadhia (Container Yard) mara baada ya Uzinduzi wa 
Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja

 Mashine ya Mobile Harbour Crane LHM 280 yenye uwezo wa kunyanyua Tani 64 ikionesha namna inavyoweza kufanya kazi katika kushusha Makontena katika Meli pia na kupanga sehemu ya kuhifadhia (Container Yard) mara baada ya Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja