Janet Jackson akiwa na mumewe Wissam Al Mana
Kwa taarifa zilizopo, mwanamuziki huyo na mumewe Wissam Al Mana, ambaye ni mfanyabiashara kutoka Qatar, wana furaha kumpata mtoto huyo waliyempa jina la Eissa Al Mana.
Janet ambaye alizaliwa Mei 16, 1966 huko Gary, Indiana na dada wa aliyekuwa mfalme wa Pop Michael Jackson, alijifungua salama bila tatizo lolote na kwamba yeye na mwanaye wanaendelea vizuri.
Mwanadada huyo aliyefunga ndoa mwaka 2012 amezipita rekodi za watu wengine mashuhuri waliowahi kupata watoto wakiwa na umri mkubwa kama vile mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry ambaye alijaliwa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47 miaka mitatu iliyopita.
Pia rekodi ya mke wa John Travolta, Kelly Preston, aliyejifungua mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.
Lakini yote hii hamfanyi Janet kuwa mwanamke wa kwanza duniani kuzaa mtoto akiwa na umri mkubwa kwani yupo Daljinder Kaur kutoka India aliyepata mtoto akiwa na umri wa miaka 70.
Daljinder Kaur (70) akiwa na mumewe Mohinder Singh (79) wakiwa na mtoto wao Arman
Sign up here with your email