Uturuki imesema
inakaribia kumtambua mtu aliyefyatua risasi hovyo na kuwaua watu 39
katika sherehe za mkesha wa mwaka mpya kwenye klabu moja ya usiku mjini
Istanbul.
Naibu waziri mkuu wa nchi hiyo , Numan Kurtulmus amesema
wapelelezi wamekwisha gundua alama za vidole pamoja na vielelezo
vingine vya mshambuliaji huyo.Kurtulmus ameongeza kuwa Uturuki itaendelea na shughuli zake za kijeshi dhidi ya kundi la IS nchini Syria,kundi linalokiri kuhusika katika shambulizi hilo la Istanbul.
Sign up here with your email