Imeelezwa kuwa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini
Awamu ya Tatu unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
utaanza rasmi kutekelezwa mwezi Februari mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo mjini Dodoma wakati akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Ameongeza kuwa, katika utekelezaji wa Mradi huo, Serikali imepanga
kuwakabidhi Wakandarasi watakaotekeleza mradi huo kwa
Wabunge ili kuhakikisha kwamba mradi husika unatekelezwa
kikamilifu.
Wakati huo huo, Kamati hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wake Dotto
Biteko imeipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa ukusanyaji wa
Maduhuli kwa kipindi cha nusu mwaka na kueleza kuwa, mwelekeo
wa ukusanyaji huo unakwenda vizuri.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akijibu hoja za Wabunge wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Medard Kalemani na Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Justin Ntalikwa wakifuatiwa na viongozi wengine wa Wizara na Taasisi zake.
Awali, akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini kuhusu
upatikanaji wa fedha na utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha
nusu mwaka kwa Kamati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Profesa Justin Ntalikwa, ameeleza kuwa, hadi kufikia Disemba
31, 2016 Wizara ilikuwa imekusanya jumla ya shilingi bilioni 201.86
sawa na asilimia 54.46 ya lengo lililokusudiwa.
“ Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato hayo yanatokana na vyanzo
mbalimbali vikiwemo ada za kijiolojia, mrahaba, ada za mwaka za
leseni, mauzo ya nyaraka za zabuni, mauzo ya gesi asilia, tozo ya
mauzo ya umeme na shughuli za utafiti wa mafuta na gesi
asilia,”amesema Prof. Ntalikwa.
Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa katika kikao cha maandalizi na kwa ajili ya vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini siku moja kabla ya kuanza kwa vikao hivyo.
Aidha, akieleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha
Julai hadi Disemba, 2016 Prof. Ntalikwa amesema kuwa, Wizara
imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kulingana na
mpango wake na kuitaja miradi kadhaa ikiwemo mradi wa
Kusafirisha Umeme Msongo wa kilovoti 400 kutoka iringa hadi
Shinyanga na kueleza kuwa, ulikamilika tarehe 28 Disemba,2016.
“ Mradi wa Kinyerezi II wenye Megawati 240 utekelezaji wake
umefikia asilimia 29 na Serikali imekwishatoa mchango wake wote
wa asilimia 15 sawa na shilingi bilioni 110 na mradi huu
unategemewa kukamilika mwaka 2018,” amesisitiza Prof. Ntalikwa.
Akizungumzia Mradi wa Kinyerezi I, Extension ya Megawati 185
ambao ni mwendelezo wa upanuzi wa Mradi wa Kinyerezi 1,
ameeleza kuwa, mradi huo unaendelea kutekelezwa na unatarajiwa
kukamilika mwaka 2018.
Akizungumzia uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Prof. Ntalikwa
amesema kuwa, ili kukuza utendaji wao, Wizara inaendelea na hatua
za uanzishwaji wa vituo vya mfano vitano katika Wilaya za Kilwa,
Mpanda, Chunya na Bukoba kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Ameongeza kuwa, vituo hivyo vitatumiwa na wachimbaji hao
kuchenjua madini yao na kujifunza namna bora ya kuendesha migodi
yao kitaalam na kwa tija zaidi.
Kaimu Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya
Nishati ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga, wa kwanza
kulia akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi, na Mtaalamu
kutoka Ewura wakibadilishana jambo kabla ya kikao na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Watendaji Wakuu wa wizara na Taasisi zilizo chini ya
Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa
(STAMIZO), Mhandisi Hamisi Komba akijibu hoja ya Wajumbe wa
kamati wakati wa kikao kati ya Wizara na Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini mjini Dodoma.
Sign up here with your email