TPSF NA DEiK YAUNDA BARAZA LA KIBIASHARA BAINA YA UTURUKI NA TANZANIA - Rhevan Media

TPSF NA DEiK YAUNDA BARAZA LA KIBIASHARA BAINA YA UTURUKI NA TANZANIA

MENGI 1

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw.Reginald Mengi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Juu ya Baraza la Kibiashara baina ya nchi ya Uturuki na Tanzania ambao ulifikiwa Tarehe 23 Januari 2017 jijini Dar es salaam.MENGI
Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw.Godfrey Sembeye akiongea na Waandishi wa habari ( hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika Serena Hotel kulia kwake ni Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi (hayupo pichani) katika Mkutano wa Baraza la Kibiashara baina ya Uturuki na Tanzani uliofikiwa Januari 23,2017 jijini Dar es salaam.MENGI 2

Bodi ya Mahusiano ya Kigeni katika Masuala ya Kiuchumi nchini Uturuki (DEiK) na Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) wameingia makubaliano ya kuanzisha baraza la kibiashara baina ya nchi hizo mbili ambayo yalifikiwa Januari 23,2017 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta binafsi Tanzania (TPSF) Bw.Godfrey Sembeye,amesema kuwa baraza la nchi hizo mbili litakuwa na majukumu na shughuli mbalimbali kwa lengo la kuimarisha uchumi na uhusiano wa kibiashara zaidi.
Bw.Sembeye ameyataja baadhi ya majukumu ambayo baraza hilo litakuwa linayasimamia kwa kusaidiana kati ya nchi hizo mbili ambayo ni:
.Kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili
.Kutoa Mchango katika kuanzisha na kukuza viwanda,kupitia ushirikiano wa teknolojia wa Mashirika na taasisi za kiuchumi za nchini Uturuki
.Kuratibu juhudi za pamoja kukusanya,kuunganisha,kuchambua,kutathmini na kueneza taarifa zinazohusu biashara,viwanda na masuala ya ushirikiano kwenye teknolojia na uwekezaji kwa manufaa ya nchi zote mbili
.Kutambua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili na kwenye ushirikiano kiuchumi na kuleta mapendekezo ya jinsi gani Serikali husika zitakavyo zitatua.
.Kuwasilisha Misaada katika kuandaa maonyesho ya kibiashara na kuhamasisha wanachama wa baraza la kibiashara kushiriki kikamilify katika shughuli za namna hizo
.Kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati ( SMEs) pamoja kuwapa ujuzi na maarifa.
.Kukusanya takwimu na taarifa juu ya fursa katika biashara,uwekezaji na masuala mengine katika ushirikiano kiuchumi, na kusambaza taarifa hii kwa wanachama.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi amesema kuwa baraza la kibiashara baina ya Uturuki na Tanzania litakuwa katika kamati za kitaifa mbili huku kila kundi litakuwa na wanachama wake na taasisi za kiuchumi au biashara.
DEiK itaunda Sekretariat ya upande wa Uturuki na TPSF na yenyewe itaunda Sekratariat kwa upande wa Tanzania na baraza kuu la biashara litahusisha Sekta mbalimbali za nchi hizo mbili na kuendelea kuangalia uwezekano wa ushirikiano zaidi kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Aidha Kamati hizo ndogo za baraza zinatarajia kukutana angalau mara moja kwa mwaka,kutazama na kujadili mafanikio ya baraza kwenye masuala ya kibiashara,uwekezaji,teknolojia baina ya Uturuki na Tanzania.
“Ikumbukwe Uturuki ni bingwa wa Kilimo hivyo watanzania watanufaika na wataweza kupata fursa mbalimbali ambazo zitawainua na kuwapeleka katika hali nzuri ya kibiashara na Uturuki hawakuzaliwa na Utajiri ila walifanya kazi kubwa mpaka kufika hapo hata sisi watanzania tuache nidhamu ya uonga”amesema Mengi.

Previous
Next Post »