MSANGI-TANROADS INABOMOA NYUMBA ZA BIASHARA 165,VIBANDA 84 MAILIMOJA KIBAHA PWANI - Rhevan Media

MSANGI-TANROADS INABOMOA NYUMBA ZA BIASHARA 165,VIBANDA 84 MAILIMOJA KIBAHA PWANI

msu1

Meneja wa TANROADS Pwani,injinia Yudas Msangi,akionekana kuzungumzia zoezi la bomoabomoa linalofanyika Mailmoja Kibaha.(Picha na Mwamvua Mwinyi)msu2
Soko la nafaka linaloendelea kubaki Mailmoja hadi hapo feb 15 mwaka huu ambapo soko kuu la eneo hilo limekumbwa na zoezi la bomoabomoa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………….

WAKALA wa barabara (TANROADS)mkoani Pwani ,umeanza zoezi la bomoabomoa kuanzia eneo la Kiluvya Darajani hadi Mailmoja-Kibaha,ambapo limefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 70 hadi sasa.
Zoezi hilo ni la siku tatu kuanzia Jan 23 hadi 25 lengo likiwa kupisha hifadhi ya barabara urefu wa mita 60.
Aidha bomoabomoa hiyo haitogusa eneo la soko la nafaka na baadhi ya mabucha ya nyama kutokana na soko jipya la nafaka kutokamilika hadi februari 15 hivyo kuendelea kusaidia wananchi kupata mahitaji yao muhimu.
Akizungumzia zoezi hilo linavyoendelea,meneja wa TANROADS Pwani,injinia Yudas Msangi,alisema wanalenga kubomoa nyumba za biashara 165,vibanda 84,nyumba za kuishi watu 10 na soko kuu la Mailmoja.
“Hadi kufikia leo mpango wetu unaenda vizuri sana ,tumeshafikia asilimia zaidi ya 70, na hii imetokana na kutokuwa na mtu wa kulalamika wala kuilaumu TANROADS”
“Tuliwapa taarifa mapema na wengi wametii kwa kuvunja wao wenyewe na kutoa vitu vyote vya thamani licha ya wachache ambao walishindwa kubomoa wao wenyewe,” alisema injinia Msangi.
Injinia Msangi,alieleza ,Maili Moja ndiyo imehitimisha zoezi la ubomoaji kwa watu waliojenga kwenye hifadhi ya barabara katika mkoa huo ambapo mwaka 2015 walibomoa maeneo mengine ya wilaya zote za mkoa.
Mkaguzi wa barabara, Injinia Livingstone Urio alisema huo ni mwendelezo wa usafishaji wa maeneo ya hifadhi ya barabara na kuweka usalama kwa wananchi kwani ni hatari kujenga ama kufanya biashara karibu na barabara.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,alisema nia ya serikali sio kuona wananchi wanatangatanga bali ni kuwajengea mazingira na miundombinu bora ili waendeshe shughuli zao .
Alieleza kwamba ,hataki kuona mtu anajipenyeza kwenye maeneo ambayo tayari yamevunjwa.
Mhandisi Ndikilo alisema, Mji wa Kibaha umeshakua na kupanuka ukielekea kuwa manispaa hivyo hainabudi kufungua mianya ya kibiashara na njia kubwa za barabara ikiwemo Kisarawe na Bagamoyo  ili kuinua soko lake.
Diwani wa kata ya Mailmoja,Ramadhani Lutambi,alimpongeza mhandisi Ndikilo kwa kushirikiana na Tanroads kutoa elimu hivyo kuepusha malalamiko ambayo huwa yakijitokeza wakati wa bomoabomoa nchini.
Alisema haijawahi kutokea zoezi kama hilo likaenda kimya kimya na watu kuondoa vifaa vyao bila shuruti kama Mailmoja.
Hata hivyo,Lutambi alisema kuna changamoto imejitokeza kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekosa maeneo soko jipya la Mnarani,ambalo limetengwa na halmashauri.
Alibainisha kuwa soko jipya ni dogo, halitoshelezi mahitaji,frem za biashara zilizobomolewa ni 165,zilizopo 110 sokoni hapo huku wajasiriamali wakiwa ni 400 na soko hilo likiwa na nafasi aya watu 200.
Lutambi alisema, lazima wengine watakosa nafasi na ndio maana malalamiko ni makubwa hivyo anawasiliana na halmashauri,wilaya na mkoa ili kuona namna ya kusaidia watakaokosa na kutenda haki bila upendeleo.
Previous
Next Post »