TAMASHA LA 14 LA SAUTI ZA BUSARA KUFANYIKA MJI MKONGWE ZANZIBAR ,FEBRUARI 9-12 MWAKA HUU. - Rhevan Media

TAMASHA LA 14 LA SAUTI ZA BUSARA KUFANYIKA MJI MKONGWE ZANZIBAR ,FEBRUARI 9-12 MWAKA HUU.

DSC_7317Mwenyekiti waTamasha la  Sauti za busara Bw.Simai M.Said wa pili kutoka kushoto akiwa anaongea na waandishi wa habari juu ya kuwataarifu kuhusiana na Tamasha la 14 la sauti za busara.
Mkurugenzi wa Tamasha la 14 la Sauti za busara Bw.Yussuph Mahmoud wa pili kutoka kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam huku akitaja baadhi ya wanamuziki ambao watatumbuiza Live.DSC_7300
Baadhi ya wageni wakisikiliza kwa makini maelezo ya Viongozi wa Sauti za busara wakati wa kutambulisha jinsi tamasha litakavyokuwa Februari 9-12 mwaka huu Mji Mkongwe visiwani Zanzibar.
Meneja wa Tamasha la 14 la sauti za busara Journey A.Ramadhani akitolea ufafanuzi suala la band Ya Moto kutokuwepo katika kutumbuiza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kujulishwa siku ya Tamasha la 14 la Sauti za busara ambalo litafanyika Mji Mkongwe Visiwani Zanzibar kuanza Februari 9-12 mwaka huu.
Wapiga picha toka katika vyombo vya habari wakifanya kazi yao kwa umakini.
Mmiliki wa blog hii ya FULLSHANGWE,Bw.John Bukuku wa kwanza kutoka kushoto akisikiliza kwa umakini mkutano wa Tamasha la 14 la Sauti za busara ambalo linatarajia kufanyika Mji Mkongwe Zanzibar kuanzia 9-12 Februari Mwaka huu.
Mwaandishi wa FULLSHANGWEBLOG,Alex Mathias wa katikati akiwa na waandishi wenzake wakifuatilia kwa umakini katika Mkutano wa Tamasha la 14 la Sauti za Busara.
…………………………..
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Tamasha la 14 la Sauti za Busara limebaki siku chache kufanyika pale Mji Mkongwe,Visiwani Zanzibar 9-12 Februari kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha la Sauti za busara lenye mbiu ya ‘AFRICA UNITED’ na litakuwa na majukwa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote wa hapa nyumbani pamoja wa Kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa Sauti za busara Bw.Simai M.Said amesema kuwa watu mbalimbali wenye rangi tofauti na umri tofauti wanatarajiwa kuunganishwa na tamasha kusherekea Muziki wa Ki-Afrika na wasanii wote watatumbuiza ‘LIVE’ Muziki wa ki-Afrika kila siku kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 7:00 usiku.
“Matarajio ya mahudhurio ni makubwa kutoka Tanzania na nje ya nchi kufatia kujaa kwa sehemu za malazi mji Mkongwe kwa wiki ya tamasha na Lengo la tamasha ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanzania ni sh 6,000 na sh 20,000 kwa siku nne za tamasha hilo”amesema Said
Aidha ndani ya siku hizo nne jumla ya wasanii 400 wa Ki-Afrika (makundi 40) yatatumbuiza tamasha la sauti za busara 2017 na litaanza na gwaride kutoka maeneo ya Kisonge ( karibu na Michezani) kuanzia saa 9:00 jioni Alhamis.
Kwa upande wa Festival Manager Bw.Journey A.Ramadhani ,amesema kuwa tamasha hili litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morocco,kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers na Shakers na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha hilo.
“Muziki unaleta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali na Duniani na ujumbe mkubwa wa Dunia ni kuwa muziki unakuza umoja na urafiki hata kwenye mipaka ya sehemu mbalimbali na kwa asilimia 100 huwa live kitu ambacho kinalifanya tamasha hilo liwe la kipekee huwapa kipaumbele wanamuziki chipukizi kutambulisha kazi zao zenye kutambulisha uhalisia wa Utamaduni”amesema Ramadhani
Hata hivyo tamasha la sauti za busara hukutanisha wataalamu wa muziki wa kimataifa na kutoa nafasi kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki ili kuwafikia watu mbalimbali dunia nzima kupitia jukwaa la sauti za wanamuziki wa nyumbani ambao hutumbuiza tamashani hupata mialiko kushiriki matamasha mbalimbali barani Ulaya na Afrika.
Aidha amesema kuwa kati ya makundi 40 nusu yatatoka Tanzania na makundi hayo ni Afrijam Band,CAC Fusion,Chibite Zawose Family,Cocodo African Music Band,Matona’s G Clef Band,Mswanu Gogo Vibes,Rajab Suleiman & Kithara,Tausi Women’s Taarabu,Usambara Sana Group,Wahapahapa Band,Ze Spirits Band.
Tuna hakika makundi kama haya yatakuwa yatawakilisha vema matamsha ya nje endapo yatapata nafasi.
Previous
Next Post »