Shirika
la Afya na elimu ya tiba Tanzania limefanikiwa kuendesha zoezi la
uchangiaji damu kwa wagonjwa wenye selimundu (Sickle Cell) Siku ya
Jumamosi Januari 21, 2017 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Mwananyamala.
Kijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) akichangia damu.
Zoezi
hili limepewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa vijana wakitanzania
kutokana na idadi ya wachangiaji damu siku hiyo ambapo asilimia 95% ya
wachangiaji damu ni vijana walio chini ya umri wa miaka 30 na asilimia
5% tu wakiwa juu ya miaka 30.
Mbali
na uchangiaji damu vijana wengi walioshiriki wametumia vyema mitandao
ya kijamii katika kuhamasisha watanzania kushiriki katika zoezi hili la
uchangiaji damu.
Zoezi
hili limelenga kuhusisha uchangiaji Damu kwa wagonjwa wa Selimundu na
hivyo kuelimisha na kuchochea uelewa juu ya ugonjwa wa Selimundu (Sickle
Cell) pia kuhimiza uboreshaji wa huduma za Afya Nchini kama inavyotajwa
katika lengo la tatu katika malengo ya maendeleo endelevu duniani
(Sustainable development Goals)
Zoezi
zima liliandaliwa na kuendeshwa na Shirika la Afya na Elimu ya Tiba
Tanzania (TAHMEF) kwa kushirikiana na Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa
Selimundu Tanzania, Vijana wa umoja wa mataifa (YUNA) na Lions Club ya
Msasani Dar es salaam.
Shukrani
Ziwafikie watanzania wote walioshiriki katika zoezi hili kwa njia
mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu
salama.
Zoezi hili linatarajiwa kuendelezwa tena kila baada ya miezi mitatu.
Muanzilishi
wa shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi (kushoto)
akiwa na Muanzilishi wa Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa selimindu
Tanzania, Arafa Said (kati) na mmoja wa vijana waliochangia damu (kulia)
Lions Club Msasani wakikabidhi mahitaji ya zoezi la uchangiaji damu kwa wanachama wa TAHMEF.
Sign up here with your email