SHULE ZA SWAZILAND ZAAGIZWA KUFUNZA UKRISTO PEKEE - Rhevan Media

SHULE ZA SWAZILAND ZAAGIZWA KUFUNZA UKRISTO PEKEE


Wizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.

Shule zimefunguliwa nchini Swaziland chini ya agizo jipya la serikali kufunza somo la dini ya kikristo pekee, hatua iliokosolewa kwa kuwa inakataa kuheshimu dini nyengine kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wizara ya elimu wiki iliopita iliwaagiza walimu wote wakuu kuhakikisha kwamba mtaala hautaji dini nyengine zaidi ya ile ya kikristo.
Kimemnukuu Sahid Matsebula, raia muislamu ambaye anafanya kazi msikitini karibu na mji mkuu wa Mbabane, kwamba sera hiyo huenda ikazua wasiwasi wa kidini katika ufalme huo.
''Serikali ina mpango gani kwa watoto wetu ambao sio Wakristo? Watafunzwa kitu kimoja nyumbani na kufunzwa kitu chengine shule''.
Sera hiyo mpya inajiri baada ya raia kulalama kwamba wahamiaji wa bara Asia na wale wa kiislamu wamekuwa wakiingia nchini humo hatua iliolazimu bunge kubuni kamati ya kuchunguza mwaka uliopita, AFP imeripoti.

Mfalme Mswati 111 wa taifa la SwazilandHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMfalme Mswati 111 wa taifa la Swaziland

Wahamiaji wengine tayari wamerudishwa makwao na waziri wa biashara Jabulani Mabuza ameambia bunge kwamba sheria itakayowazuia wahamiaji kuanza biashara nchini Swaziland imeanza kubuniwa.
Stephen Masilela, rais wa baraza la makanisa nchini humo ameunga mkono mtaala huo mpya.
''Ukristo ndio msingi wa kujengwa kwa taifa hili''.
Taifa la Swaziland linaloongozwa na mfalme Mswati wa tatu tangu 1986 lina idadi ndogo ya waislamu.
Sera hiyo ya kufunza dini ya kikristo pekee katika shule pia imekosolewa na mwandishi Nomsa Mbuli wa gazeti la Times of Swaziland:Kinachoinua dini moja juu ya nyengine ni nini wakati ambapo katiba inaagiza usawa wa kidini?
Previous
Next Post »