KENYA KUNUNUA NDEGE 14 ZA KIJESHI KUTOKA MAREKANI - Rhevan Media

KENYA KUNUNUA NDEGE 14 ZA KIJESHI KUTOKA MAREKANI

Kenya yanunua ndege 14 za kijeshi kutoka MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKenya yanunua ndege 14 za kijeshi kutoka Marekani
Serikali ya Marekani imeidhinisha mpango wa kuliuzia jeshi la Kenya ndege 14 za kijeshi zenye thamani ya dola milioni 418, Idara ya ulinzi nchini humo imetangaza.
Ndege hizo zitatumika katika vita dhidi ya wapiganaji wa al-Shabab wenye makao yao huko nchini Somalia ambao wamefanya mashambulizi mbaya zaidi nchini Kenya, idara hiyo imeongezea.
Imesema kuwa ndege hizo kwa jina Air Tractor zitaweza kukabiliana na wapiganaji hao kwa karibu ikilinganishwa na ndege za sasa za f-5 fleet.
Mauzo hayo yanachangia sera ya kigeni ya usalama ya taifa la Marekani kwa kuwa Kenya inaongoza katika eneo hilo katika vita dhidi ya wapiganaji hao.
Previous
Next Post »