SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO - Rhevan Media

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

……………………………………………………………Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali
haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo.
Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga
kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu
kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo
wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.
Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na
kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa
macho

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu
wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta
manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu
wachache


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi  ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo
badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo


Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea
katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori
tengefu katika wilaya hiyo.
Previous
Next Post »