Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara baada ya kukagua jengo jipya la abiria (Terminal III) lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mradi wa jengo jipya la Terminal III lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Eng. Mohamed Milanga (Katikati) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akikagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo jipya la Abiria (Tb III) lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA, Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Bw. Salim Msangi akisoma taarifa ya utekelezaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) kuhusu Ujenzi wa jengo jipya la abiria (Tb III), lililopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere JNIA. Jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………
Serikali imesema itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya pili Serikali itatoa fedha ili kukamilisha mradi huo.
”Awamu ya kwanza ya ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani” amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwenda sabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier Q400.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi , amesema mpaka mwishoni mwa mwanzoni wa Mwaka huu mradi huo umekamilika kwa asilimia 66 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuezeka na kumalizia kazi za ndani ya jengo ikiwemo usimikaji wa mitambo ya umeme, viyoyozi na utandikaji wa nyaya na mbomba kwa ajili ya miundombinu ya ndani.
Ameongeza kuwa kazi za nje ya jengo zinazohusisha maegesho ya ndege yamekamilika kwa asilimia 53, maegesho ya magari asilimia 36 na eneo la mitambo na umeme asilimia 46.
Bw. Msangi amesema kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha JNIA watafikia milioni 5 kwa mwaka na makadirio ifikapo mwaka 2025 idadi itaongezeka watafiia milioni 5 kwa mwakaa.
Mradi huu wa jengo la mita za mradi za mraba sitini elfu unatarajiwa kukamilikak mwezi Desemba Mwaka huu na utahudumia abiria zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na litaweza kuhuduumia abiria 2,700 kwa saa na litakuwa na uwezo wakuhudumia ndege kubwa aina ya Airbus A380.
Sign up here with your email