Kufuatia kuenea habari katika mitandao ya mbalimbali ya kijamii inayomhusu Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji kuwa amefanya mahojiano na kituo cha redio cha Times FM kuhusu pesa za tetemeko la ardhi, kituo cha Times FM kimekanusha habari hizo.
Katika taarifa ambayo imetolewa na kituo hicho cha redio kupitia kurasa zake za Facebook na Instagram, Times FM wamesema kuwa si kweli kuwa wamefanya mahojiano wala kurusha habari zozote ambazo zinamhusu MO Dewji na wanafanya uchunguzi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Sign up here with your email