KUTOKA MAKTABA: Video ikimuonesha Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo eneo ya Ubungo jijini Dar es salaam miaka minne iliyopita akiwa na aliyekuwa waziri wa Ujenzi wakati huo Dkt. John Pombe Magufuli ambaye sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kesho tarehe 25 /01/2017 anatarajiwa kuzindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit - BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani jijini Dar es salam.

Uzunduzi huo utahudhuriwa na Rais wa
Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop na Mkurugenzi Mkazi wa Benki
ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird.
Awamu ya Kwanza ya mradi wa ujenzi wa
Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) yenye urefu wa kilometa 20.9
unaojumuisha barabara ya Kimara – Kivukoni, Magomeni - Morocco na Fire – Kariakoo ulikamilika
Desemba 2015.
Aidha, utoaji wa huduma ya Mabasi Yaendayo
Haraka ulianza tarehe 10 Mei, 2016. Kwa sasa huduma ya mabasi katika kipindi
cha mpito inatolewa katika njia nane, vituo vikuu vitano, vituo vidogo 28 na
karakana moja kwa kutumia mabasi 140 yanayojumuisha mabasi makubwa 39 yenye
uwezo wa kubeba abiria 160 kila moja na mabasi madogo 101 yenye uwezo wa kubeba
abiria 60 kila moja.
Mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi
Yaendayo Haraka (BRT) umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita kwa lengo la
kupunguza msongamano wa magari katika Jiji
la Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU
MKUU (UJENZI)
24 Januari, 2017
Sign up here with your email