KUTOKA UGAIBUNI : MCHEKESHAJI ALIYE MFANYIA UTANI MWANA WA TRUMP ASIMAMISHWA KAZI - Rhevan Media

KUTOKA UGAIBUNI : MCHEKESHAJI ALIYE MFANYIA UTANI MWANA WA TRUMP ASIMAMISHWA KAZI

Donald Trump Washington. Picha: 20 Januari 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBarron, 10, (kushoto) ndiye kitinda mimba wa Donald Trump
Mwandishi wa vichekesho wa kipindi cha Saturday Night Live nchini Marekani amesimamishwa kazi baada ya kuandika ujumbe uliomkejeli mwana wa Rais Donald Trump, Barron, kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Vyombo vya habari Marekani vimemnukuu mtu anayefahamu mambo ya ndani ya SNL akisema Katie Rich amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana.
NBC, wanaopeperusha kipindi hicho, bado hawajatoa taarifa yoyote rasmi kuhusiana na hilo.
Bi Rich aliandika ujumbe kwenye Twitter Ijumaa akisema: "Barron atakuwa mtu wa kwanza mshambuliaji hapa nchini aliyepokea elimu yake nyumbani."
Ujumbe huo wa mzaha unaonekana kutania suala la matumizi ya silaha Marekani, ambapo kumeripotiwa visa kadha vya raia wa Wamarekani kuwaua watu wengi kwa kuwapiga risasi.
Kinyume na ujumbe unavyoashiria, Barron hahudhurii masomo yake nyumbani bali husomea shule ya kawaida.
Bi Rich alishutumiwa vikali mtandaoni kutokana na ujumbe huo.
Saa chache baadaye aliufuta ujumbe huo na kuufanya ukurasa wake wa Twitter kuwa wa faragha.
Bi Rich alirejea mtandaoni Jumatatu na kuomba msamaha.
Katie Rich's tweets her apologyHaki miliki ya pichaTWITTER
Ujumbe mmoja kwenye Facebook wa kujibu ujumbe wa kwanza wa Bi Rich umesambazwa karibu mara milioni tatu kwenye mtandao huo wa kijamii.
Ujumbe huo unasema: "HAKUNA mtoto anayestahili kuzungumziwa kwa njia kama hiyo...Yeye ni mtoto, anafaa kuheshimiwa na hafai kuingiliwa".
Chelsea Clinton, ambaye aliwahi kuishi ikulu kama mtoto, amemtetea Barron.
Chelsea Clinton's tweet about Barron Trump.Haki miliki ya pichaTWITTER
SNL wameandaa vipindi kadha miezi ya karibuni wakimkejeli Rais Trump.
Bw Trump, aliyeapishwa tarehe 20 Januari, amesema kipindi hicho "hakichekeshi" na waigizaji wake ni "wabaya sana".
Previous
Next Post »