Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Salum
Mayanga (kulia) kuwa kocha wa muda (Interim coach), wa timu ya taifa ‘Taifa
Stars’.
Kocha Salum Mayanga, ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface
Mkwasa (pichani chini) ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.
Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya
Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019
ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.
Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha
wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi
katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango
yake inayofuata.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Sign up here with your email