Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Mmiliki
mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya
hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili
mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.
Washtakiwa
wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na
Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.
Wakili wa
serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa
nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia
ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao na waliamua
kushindwakutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.
Hata hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa
mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
Mpaka sasa
washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi ya Milioni 10
kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.
Maxence Melo akijaribu kumueleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao
Sign up here with your email