MLANGUZI '' EL CHAPO '' GUZMAN AHAMISHWA KUTOKA MEXICO HADI US - Rhevan Media

MLANGUZI '' EL CHAPO '' GUZMAN AHAMISHWA KUTOKA MEXICO HADI US

Joaquin GuzmanHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJoaquin Guzman anayefahamika sana kama El Chapo, kwa Kiingereza Shorty
Kiongozi wa genge la walanguzi wa mihadarati nchini Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman amehamishwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa serikali nchini Marekani, serikali za nchi hizo mbili zilitangaza Alhamisi.
Aliwasili mjini New York kwa ndege kutoka Cuidad Juarez.
Bw Guzman, ambaye huenda akafungwa jela maisha nchini Marekani, amekuwa akisakwa na maafisa wa Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.
Anadaiwa kuingiza kiasi kikubwa sana cha dawa za kulevya nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa genge la Sinaloa alikuwa anakabiliwa na maombi mawili ya kutaka apelekwe Marekani kujibu mashtaka - moja kutoka California na jingine Texas.
Mwaka uliopita, alihamishiwa gereza la Ciudad Juarez, ambalo linapatikana maeneo ya mpakani karibu na mji wa El Paso katika jimbo la Texas.
Maafisa hata hivyo walikanusha tuhuma kwamba hatua hiyo ilikuwa kama maandilizi ya kumhamishia Marekani.
Bw Guzman amekuwa akipigania kusalia Mexico lakini rufaa zake zilikataliwa.
Amekuwa akilindwa vikali gerezani ikizingatiwa kwamba alikuwa ametoroka magereza mawili ya ulinzi mkali awali.
Anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya dola mjini Brooklyn Ijumaa.
Ciudad JuarezHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Mexican wakishika doria uwanja wa ndege wa Ciudad Juarez, Guzman alipokuwa anasafirishwa

Matukio makuu

Februari 2014: Akamatwa baada ya kuwa mtoro kwa miaka 13, baada ya kutoroka kutoka jela ya Puente Grande akiwa amejificha ndani ya kapu la nguo
Julai 2015: Atoroka kutoka Altiplano kupitia njia ya chini kwa chini
2 Oktoba 2015: Ahojiwa na mwigizaji mmarekani Sean Penn mafichoni jimbo la Durango, kisha kwa simu na video
17 Oktoba 2015: Maafisa wa Mexico watangaza walikaribia kumkamata akiwa jimbo la Sinaloa
Januari 2016: Akamatwa akiwa Los Mochis, Sinaloa
Mei 2016: Jaji wa Mexico aidhinisha kuhamishiwa kwake Marekani
Oktoba 2016: Jaji nchini Mexico akataa rufaa yake
Previous
Next Post »