Mfanyakazi katika kivuko kikuu cha feri nchini Gambia, ameiambia BBC kuwa maelfu ya watu wanaikimbia nchi kila siku wakihofia kutokea vita.
Adama Barrow alishinda uchaguzi na kuapishwa kwake kunapangwa kufanyika siku ya Alhamisi.
Lakini Rais Yahya Jammeh aliyakataa matokeo hayo na amesema kuwa hataondoka madarakani hadi pale mahakama ya juu itakaposikiliza kesi.
Bunge limekutana kwa kikao cha dharura. Huku sababu ya kikao hicho ikiwa haijulikani, mwandishi wa BBC mjini Banjul anasema kuwa bunge huenda likaombwa kuongeza muhula wa bwana Jammeh.
Bwana Barrow atabaki nchini Senegal hadi siku ya kuapishwa kwake.
Gambia, nchi yenye watu wasiozidi milioni mbili inazungukwa pande tatu na Senegal, ambayo inasema kwa inatathmini kuchukua hatua za kijeshi kumuondoa bwana Jammeh madarakani.
Sign up here with your email