BURUNDI KUANZA KUONDOA WANAJESHI SOMALI - Rhevan Media

BURUNDI KUANZA KUONDOA WANAJESHI SOMALI

Burundi ina wanjeshi 5,400 katika kikosi cha AmisonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBurundi ina wanjeshi 5,400 katika kikosi cha Amison
Ofisi ya Rais nchini Burundi imetaka rasmi wizara ya ulinzi na ile ya mashauri ya nchi za kigeni, kuanza mchakato wa kuondoa wanajeshi wake kutoka nchini Somalia.
Burundi, iliyo na wanjeshi 5,400 katika kikosi cha Amison, ndiyo ya pili kwa kuchangia wanajeshi wengi zaidi katika kikosi cha muungano wa Afrika ambacho hufadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya.
Lakini imeamua kuondoa wanajeshi wake kufuatia uamuzi wa EU wa kusitisha malipo kwa serikali ya Burundi ya Uro milioni tano kila mwezi kama mshahara wa wanajeshi hao.
Uchaguzi wa urais uliokumbwa na mzozo wa mwezi Aprili mwaka 2015, ambapo rais Nkurunziza aliingia mamlakani kwa muhula wa tatu, umesababisha Burundi kuwekewa vikwazo na mashirika ya kimataifa ikiwemo EU.
Mwezi Novemba mwaka uliopita, Muungano wa Afrika ulipinga uamuzi wa EU wa kusitisha malipo ya mishahara kwa wanajeshi hao kupitia kwa serikali, ukionya kuwa ingekuwa na madhara kwa kikosi cha Amisom.
Previous
Next Post »