Wamiliki hao na wasafirishaji wengine mwaka jana walikuwa wakilalamika kukosekana kwa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na wengine kulazimika kuyaegesha malori yao.
Akizungumza jana na gazeti hili, Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), Rahim Dosa alisema, “tunaanza kuona matumaini mbele yetu.”
Alisema wameanza kupata mizigo ingawa hali bado si shwari, lakini imeanza kuongezeka kuanzia Desemba mwaka jana na Januari mwaka huu.
“Tunaomba Mungu hali hii iendelee ili tuweze kufanya biashara kama ilivyokuwa zamani,” alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mizigo Bandarini (Taffa), Tony Swai alisema mizigo bandarini imeanza kuongezeka.
Sign up here with your email
