MABILIONI YAIBIWA KWA JAJI MATUNGI - Rhevan Media

MABILIONI YAIBIWA KWA JAJI MATUNGI

MAMILIONI ya shilingi ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yaliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa nchini, hayajulikani yalipo, 

“Ama mamilioni hayo yamekwapuliwa au yametumika isivyopasa,” MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa kutoka ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinasema, mamilioni hayo ya shilingi yaliingizwa katika akaunti ya Msajili katika benki lakini sasa hayajulikani yalipo au yalivyotumika.
Mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya ofisi ya waziri mkuu ameliambia gazeti hili kuwa tayari uchunguzi umeanza ili kufahamu jinsi  fedha hizo zilivyotumika.
Mtoa taarifa huyo anasema, “kuyeyuka” kwa fedha hizo kuligunduliwa na mkaguzi wa ndani wa ofisi hiyo.
Amesema, “ofisi ya msajili ilipokea Sh. 600 milioni ili zitumike kujengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa; lakini kazi hiyo haijafanyika.”
Amesema, “…baada ya kubaini kutokuwepo fedha hizo au ushahidi wa matumizi yake, ndipo ikaagizwa ufanyike ukaguzi maalum ili kupata uhakika wa kile kilichoonwa na mkaguzi wa ndani.”
MwanaHALISI lilipomuuliza Jaji Francis Mutungi juu ya madai ya kupotea kwa mamilioni hayo ya shilingi, alikiri kuwapo ukaguzi katika ofisi yake kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.
Previous
Next Post »