MAAMUZI YA TFF KWA JERRY MURRO JUU YA MSAMAHA WAKE KWA RAIS MALINZI - Rhevan Media

MAAMUZI YA TFF KWA JERRY MURRO JUU YA MSAMAHA WAKE KWA RAIS MALINZI

jamal-malinzi-1rrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrShirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limekanusha kupokea barua ya kuomba msamaha kutoka kwa Afisa habari na Mawasiliano wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam,JerryMurro ambaye alifungiwa mwaka jana kutumikia kifungo cha mwaka moja kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Akizungumza na FULLSHANGWEBLOG,Msemaji wa TFF Alfred Lucas,amesema kuwa pamoja na kuenea kwa taarifa zinazodai kuwa Murro aliandika barua ya kuomba kusamehewa adhabu hiyo ni kuwa bado TFF haijapata rasmi barua ya maandishi kutoka kwa msemaji.
Aidha Lucas amesema kuwa wao wenyewe wamemsikia Murro akizungumza kwenye vyombo vya habari juu ya kuomba msamaha kwa Rais wa TFF,Jamal Malinzi  ili ampatie msamaha kwa makosa ambayo yalimtia nyundo ya adhabu ya mwaka moja msimu uliopita.
“Mimi mwenyewe nimemsikia Murro akisema kuwa amekwenda moja kwa moja kwa Rais kupeleka barua yake ya kuomba msamaha huku pia nataka niwaweke wazi watanzania kuwa kama Murro angekuwa ameleta barua yake kwa mtu yeyote katika Ofsi za TFF hapa Karume basi tungekuwa na taarifa hizo kwa sababu sisi ndio watendaji na muda wote tupo hapa Ofsini”amesema Lucas
Ikumbukwe kuwa Murro alifikishwa mwaka jana katika kamati ya maadili kwa makosa matatu na baadae alikuja kubainika kuwa alitenda makosa mawili kubwa zaidi lilikuwa ni la kutoa matamshi Makali kwa Viongozi wa TFF.
Hata hivyo amesema Ofsi za TFF zipo wazi muda wote kwa siku za kazi na kama barua hiyo itawafikia wataipeleka moja kwa moja kwa wahusika ili kuangalia uwezekano wa kufanyia kazi maombi yake hayo.
Previous
Next Post »