DC WA WILAYA YA UYUI AACHIA NGAZI - Rhevan Media

DC WA WILAYA YA UYUI AACHIA NGAZI

DC UYUI 2Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka  Waandishi  waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu.”Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.
Previous
Next Post »