Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa bongofleva nchini, Judith Wambura "Lady Jaydee" (Binti Komando) amesema kuwa wanamuziki wa kike wanatakiwa kuongeza nguvu na kutokata tamaa katika kazi zao.
Jaydee ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na ripota wa globu ya jamii juu ya nini wasanii wakike wanatakiwa kufanya ili kufikia mafanikio ambayo yeye ameyafikia katika muziki huu ndani na nje ya nchi.
“Muziki wa sasa unazidi kukua na wasanii wa kike wanajitahidi ila wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi ya hapo, hivyo sisi tulio tangulia tunatakiwa kuwatia moyo pia wasikate tamaa kwani vipaji wanavyo na wameonyesha na jamii imewakubali”Amesema Jaydee.
Amesema kuwa kuna kipaji na kufahamika ni jambo jingine na kutunza kipaji chako kutokana na misukosuko ni jambo jipya ambalo linaweza kukukatisha tama katika muziki wa leo.
Amesisitiza kuwa katika kipindi hiki kumekuwa na wanamuziki wengi wa kike tofauti na miaka yetu ambayo tulikuwa tukiesabika lakini wingi huo bado hauwezi kulinganishwa na wingi wa wanamuziki wa kiume jambo ambalo linawapa ushindani mkubwa wanamuziki wa kike.
Ametaja kuwa licha ya kupata nafsi lakini bado wanamuziki hao wanapitia changamoto kubwa sana ya kujikwamua kiuchumi kutokana na muziki.
UNAWEZA ANGALIA HAPA CHINI VIDEO YAKE MPYA
UNAWEZA ANGALIA HAPA CHINI VIDEO YAKE MPYA
Sign up here with your email