KIUNGO HULL CITY AVUNJIKA FUVU LA KICHWA - Rhevan Media

KIUNGO HULL CITY AVUNJIKA FUVU LA KICHWA


Kiungo wa klabu ya Hull City ya nchini Uingereza, Ryan Mason amefanyiwa upasuaji, baada ya kuvunjika fuvu la kichwa, kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, dhidi ya Chelsea, Jumapili.

Mlinzi wa Chelsea Gary Cahill (kulia) alipogongana kichwa na Ryan Mason wa Hull City

Mason, mwenye umri wa miaka 25, aligongana na mlinzi wa Chelsea, Gary Cahill dakika ya 13 ya mchezo huo, ulioisha kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, uwanja wa Stamford Brdidge.
Baada ya dakika 8 za matibabu uwanjani, Mason aliwekwa hewa ya oxygen na kutolewa uwanjani kwa machela, kisha kukimbizwa Hospitali ya St. Mary's Hospital mjini London.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hull, imesema kuwa Mason, anaendelea vizuri, na atabakia hospitali kwa siku kadhaa.
"Ryan yupo kwenye hali nzuri na anatarajiwa kubaki hospitalini kwa siku chache zijazo," ilisema taarifa ya Hull.
Previous
Next Post »