HATARII : SANGARA WAZIDI KUWA ADIMU MWANZA - Rhevan Media

HATARII : SANGARA WAZIDI KUWA ADIMU MWANZA

Wavuvi wakiwa katika harakati za kutafuta Samaki Ziwa Victoria

UZALISHAJI wa Samaki katika Kiwanda cha Tanzania Fish Processors Limited (TFP), jijini Mwanza, kinachojihusisha na uchakataji wa minofu ya samaki aina ya Sangara umeshuka kutoka tani 120 kwa siku hadi Tani 25, 
Kushuka kwa uzalishaji wa samaki katika kiwanda hicho kunatokana na ukosefu wa malighafi ya samaki, unaochangiwa na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria.
Godfrey Samwel Meneja rasilimali watu wa kiwanda hichoameiambia Kamati ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira iliyotembelea kiwandani hapo kuwa kushuka kwa uzalishaji huo kutachangia kushuka kwa mapato ambapo mwaka 2016 kiwanda hicho mapato kiliingiza Dola za Kimarekani 30 millioni.
Kiwanda hicho kilichosajiliwa mwaka 1992 na kuanza shughuli zake mwaka 1996, kimelazimika kutembelea sehemu mbalimbali na kutoa elimu kuhusu madhara ya uvuvi haramu na namna ya kupata mavuno bora ya samaki ili kukabiliana na tatizo la kupungua kwa samaki.
“Kiwanda hiki kimetoa ajira kwa watu 300, lakini pia kimekuwa kikijihusisha na utunzaji wa mazingira na tunazingatia sheria zote za nchi na za kimataifa katika utunzaji wa mazingira na kuzalisha taka ngumu na majitaka,” amesema Samwel.
Dalaly Kafumu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira, amekitaka kiwanda hicho kuongeza juhudi  katika utunzaji wa mazingira huku akidai Serikali inaendelea na jitihada za kupambana na uvuvi haramu ili kuongeza uzalishaji katika viwanda vinavyochakata Samaki nchini.
Previous
Next Post »